Wilaya ya Namtumbo ina utajiri wa madini ambayo bado hayajawekewa uwekezaji, Madini yanayopatikana kwa sana Wilayani Namtumbo ni Urania (Uranium) ambayo yanapatikana Mto mkuju uliyopo kaya ya Likuyuseka, Mpaka sasa ni kampuni moja tu ya Mantra iliyoanza kuchimba madini ya Uranium katika mto mkuju uliopo kilometa 90 kutoka wilayani Namtumbo.
Urania
Sheria ya madini ya mwaka 1998 kifungu cha 24-29 kinaelezea juu ya taratibu na Leseni ya uchimbaji wa madini, ambapo Wilaya ya Namtumbo imejipanga kufungua ofisi ya madini kwenye makao makuu ya Wilaya kwaajili ya kutoa fursa zaidi juu ya uwekezaji katika sekta hii muhimu ya Madini.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.