HALMASHAURI MKOA WA RUVUMA ZATAKATA KWA HATI SAFI
Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma Kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 zimepata hati safi Kwa mujibu wa taarifa za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali (CAG).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Rehema Madenge Pamoja na viongozi mbalimbali Mkoani Ruvuma walizipongeza Halmashauri zao Kwa kupata hati safi.
Pamoja na pongezi hizo Madenge aliziagiza Halmashauri kutobweteka na kupata hati safi Bali zijikite kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za fedha ili kuzuia hoja zisijitokeze.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Pamoja na kuwashukuru wataalamu wake Kwa kusimamia kanuni,sheria na taratibu za fedha iliyopelekea Halmashauri hiyo kupata hati safi aliahidi kuongeza ushirikiano na wataalamu wake ili kuzuia hoja zisizo za lazima zisijitokeze na kuyafanyia kazi mapendekezo ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali ili Halmashauri yake iendelee kupata hati safi Kila mwaka.
Wakuu wa Wilaya Mbinga,Tunduru,Namtumbo ,Songea na Nyasa Kwa upande wao walizipongeza Halmashauri zao Kwa kupata hati safi na kudai tafsiri ya hati safi ni kuashiria uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma.
Halmashauri nane zilizopata hati safi katika Mkoa wa Ruvuma ni Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,Namtumbo,Nyasa,Mbinga , Halmashauri ya Mji wa Mbinga Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Madaba.
Taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali zilisema Halmashauri hizo za Mkoa wa Ruvuma zilikidhi vigezo vya kupata hati safi baada ya kujibu hoja na kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 na kujipatia hati safi .
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.